Leo October 17, 2016 Nimeipata hii
kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu kuutaarifu umma juu ya
utapeli unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa
kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la
kupatiwa malipo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya
Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT imeelezwa
kuwa utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma
ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.
Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa
ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo
wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa
vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT hutolewa na Makao Makuu ya JKT kwa
mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na
tovuti ya JKT.
Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi
kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa
EmoticonEmoticon