Wednesday, July 06, 2016

Wafanyakazi wa serikali Nchini Zimbabwe wagomea shughuli zote za kiserikali nchini humo

Nchini Zimbabwe wafanyakazi wa serikali wamesusia kwenda kazini,wanaharakati wametaja kuwa ni kususiwa kwa shughuli zote za kitaifa.
Maandamano hayo yanatokana na hali mbaya ya kiuchumi nchini humo.
Mitaa ya miji mikuu nchini Zimbabwe imetulia tulii, maduka na masoko yamefungwa.
Kampeni ya kuwataka raia wa taifa hilo kusalia makwao ilianza kwenye mitandao ya kijamii, kutokana na ufisadi unaoendelea , pamoja na usimamizi mbaya wa uchumi wa taifa hilo.
Mitandao ya kijamii ilizimwa kwa kipindi cha saa nne.
Maandamano yalianza wiki iliyopita karibu na mpaka wa taifa hilo na Afrika Kusini, baada ya sheria ya kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa nyingi kutoka Afrika Kusini kuanza kutekelezwa.
Maandamano ya leo ndio makubwa zaidi kuwai kufanyika nchini Zimbabwe dhidi ya serikali.
Maandamano hayo yanafuatia mgomo wa madaktari na wauguzi.
Aidha maandamano ya madereva wa teksi na wafanyibiashara dhidi ya vizuizi vya polisi ambavyo wanadai huwa ni vituo vya kudai hongo.
Visa vingi vya ukiukaji wa haki za kibinadamu vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi dhidi ya umma vilichapishwa katika mitandao ya kijamii.
Kwa sasa mgogoro wa kiuchumi unashuhudiwa nchini humo, na kupelekea uhaba mkubwa wa pesa.
Wafanyikazi wa umma wamekataa kurejea kazini pasi na kulipwa malimbikizi ya mishahara yao.
Kampeini hiyo inadaiwa kuanzishwa na kasisis mmoja Ivan Mawareery ambaye aliwataka Wazimbabwe wavalie mavazi yenye rangi za bendera ya taifa kama njia yao ya kulalamikia kudhulumiwa kwa haki zao za kimsingi.

No comments:

Post a Comment