kilimo cha mbogamboga kinavyo weza kuinua uchumi wa wakulima wadogo wadogo katika maeneo ya mijini na vijijini picha na Emmanuel Richard.
Kilimo ni Sekta muhimu kwa maisha
na uchumi wa wakazi wa Mjini na pembezoni mwa Mji.
|
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa
Mikoa ambayo Kilimo huchangia katika kuongeza kipato kwa wakazi , upatikanaji
wa chakula (lishe bora) na hifadhi ya mazingira. Takribani asilimia
thelathini (30%) ya mazao ya kilimo yanayotumiwa na wakazi wa Jiji huzalishwa
katika maeneo mbalimbali katikati na pembezoni mwa Jiji.
Mboga za majani na matunda ni mazao muhimu
yanayozalishwa kutokana na kuwa karibu na soko (walaji) na bei nzuri .
Mboga zinazozalishwa ni mchicha,
matembele, chainizi kabichi, bamia, kisamvu, sukuma wiki, bilinganya, uyoga,
mnavu, kisamvu na maboga . Matunda ni pamoja na makakara, matango, papai,
nanasi, matikiti maji, na machungwa .
Pamoja na hayo kilimo kinahitaji teknolojia na maandalizi mazuri ilikuweza kupata matokeo mazuri katika kilimo Nchini Tanzania
|
EmoticonEmoticon